KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMA E-mail: dvdmwk6@gmail..com SIMU: 0713 084 360

Wednesday, June 17, 2015

BENKI YA NMB YAZINDUA RASMI FAMILIA YA KADI ZA BENKI “MASTERCARD DEBIT” ZINAZOKUBALIKA KIMATAIFA.

 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa (katikati) pamoja wakurugenzi wa Benki ya NMB wakikishangilia kikundi cha sanaa kilichotumbuiza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumika kwa mara ya kwanza kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

 Wadau wa benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback, akiwahutubia wadau wa Benki ya NMB wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi hiyo mpya ambayo itaanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (katikati) pamoja na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback, (kulia) wakiteta jambo kabla ya uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumika katika benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo hivi karibuni. (Anayeangalia kulia) ni Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Prof. Joseph Semboja. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam.

 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya NMB, Prof. Joseph Semboja mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam rasmi kwa kuzindua huduma mpya ya Mastercard iliyoanzishwa na benki hiyo.(Katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker.

 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin W. Mkapa (kushoto) akisalimiana na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback (kulia) mara tu alipowasili katika uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo. (Katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker

 Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam . 

 Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumika hivi karibuni kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam. 

 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa akihutubia wadau wa benki ya NMB kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Mastercard ya benki ya NMB ambayo itatumika rasmi kwa wateja wake hivi karibuni. Hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro Hotel.