Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC)
imezindua huduma mpya ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM jijini Dar es
Salaam katika juhudi za benki hiyo kuboresha huduma za kifedha nchini.
Kuanzishwa kwa huduma hiyo kunathibitisha
malengo ya benki hiyo ya kutoa huduma sahihi na ya wakati kwa wateja wake
nchini nzima na huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM itakuwa
ikipatikana masaa 24 kila siku.
“Uanzishwaji wa huduma hii ya kuweka
fedha kwenye mashine za ATM itawahakikishia wateja wetu kupata huduma sahihi na
ya uhakika wakati wowote, uwekaji wa fedha katika mashine hizi ni wa haraka,
rahisi, na inaokoa muda wa kupanga foleni ndani ya benki,” alisema Mkuu wa Njia
Mbadala za Kibenki wa NBC, Raymond Mutagahywa.
Aliongeza kwamba huduma hii ya NBC
kwa mtumiaji yeyote ni ya kirafiki na rahisi sana ni kwamba mtu anahitajika
kufanya mambo machache tu baada ya kuingiza kadi yake ya ATM na kuchagua sehemu
ya kuweka fedha na mashine ya ATM itafunguka ili mteja aweze kuweka fedha zake.
Benki hii ya NBC imeanza huduma hiyo
kwenye matawi yake ya jijini Dar es Salaam, karikaoo, kinondoni, Mlimani City
na Tawi la Makao makuu ambayo mteja anaweza kuweka mpaka shilingi za kitanzania
1.5milioni kwenye mashine za ATM.
Uzinduzi huu wa kuweka fedha kwenye
mashine za ATM ulifanyika katika Tawi la benki hiyo la Mlimani city na
kushuhudiwa na wateja kadhaa wa benki hiyo na walivutiwa na jisni mashine
zinavyotumika kuweka fedha moja kwa moja.
“Hizi mashine za ATM zimekuja wakati
muafaka kabisa hasa kwa wateja wetu ambao wanaendelea na biashara zao wakati
ambao matawi mengi yamekuwa yamefungwa lakini huduma hii itawawezesha kufanya
shughuli zao za kibenki za kuweka fedha bila matatizo,’ aliongeza Neema Munisi
Mhasibu wa Tawi la Mlimani City.
“Tumeanzisha na kuzindua huduma hii
ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM kwenye matawi manne tu jijini Dar es
Salaam na tutaendelea kufungua na kusambaza huduma hii ya kuweka fedha kwenye
mashine hizi nchini nzima,” aliongeza Munisi
Kwa wake Mteja wa benki hiyo
aliyejaribu huduma hiyo mpya, Franscis Xavier Momanyi alisema kwamba kwa huduma
hiyo mpya kutoka benki hiyo itawahikishia wateja wote uhakika wa kupata fedha
au kuweka fedha wakati wowote pindi watakapohitaji.
Alisema kwamba ni muhimu kwa benki
hiyo kupeleka kwa haraka huduma hiyo ya kipekee kwenye matawi mengine nje ya
mkoa wa Dar es Salaam ili wateja wengine wapate fursa ya kutumia huduma hiyo.