|
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira wa Wavu Tanzania (Tava) Muharami Mchume akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mashindano ya kwanza ya taifa ya mpira wa wavu katika hoteli ya Mbalamwezi
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
|
|
Vingozi wa Tava, wadhamini wa
mashindano hayo kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa wavu wa
ufukweni Mikocheni jijini Dar es Salaam.
|
Mkurugenzi wa kinywaji cha Black
Energy Amar Shanghavi (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano
ya kwanza ya taifa ya mpira wa wavu Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
mwenyekiti wa Tava augustino Agapa na kulia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa
wavu mkoani Dar es Salaam Mwasha.
Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu
ya wanawake ya Tanzania Prisons Hellen Richard (kushoto) akiokoa mpira huku
mwenzake Everyinne Alberth akiwa tayari kumsaidia wakati walipocheza na Jeshi
Satrs katika mchezo wa fainali ya mashindano ya kwanza ya wazi ya taifa ya wavu
wa ufukweni juzi jijini Dar es Salaam. Prisons ilishinda 2-0 na kutwaa ubingwa.
|
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa
Wavu Tanzania (Tava) Augustino Agapa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Jeshi
Stars kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mpira wa wavu wa ufukweni ya
mashindano ya wazi ya taifa kwenye ufukwe wa hoteli ya Mbalamwezi Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
|
|
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tava) Augustino Agapa akisalimiana na mchezaji
wa timu ya Tanzania Prisons Everline Alberth kabla ya kuanza kwa mchezo wa
fainali ya mpira wa wavu wa ufukweni ya mashindano ya wazi ya taifa kwenye
ufukwe wa hoteli ya Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam. Prisons
walishinda seti 2-0. (Na Mpiga Picha Wetu).
|
|
Hellen Richard (mbele) wa timu ya
mpira wa wavu ya Tanzania Prisons na wachezaji wa Jeshi Stars Liza John
(kushoto) na Zuhura Ally wakati wa fainali ya mchezo wa wavu wa ufukweni
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
|
|
Mkurugenzi wa Kampuni ya Black
Energy Amar Shanghavi akisalimiana na mchezaji wa timu ya mpira wa wavu ya
Jeshi Stars Ford Edward kabla ya kuanza kwa fainali ya mashindano ya wazi ya
taifa ya wavu wa ufukweni dhidi ya Karafuu ya Zanzibar jijini Dar es Salaam.
Karafuu walishinda seti 2-0.
|
|
Mkurugenzi wa Kampuni ya Black
Energy Amar Shanghavi akisalimiana na mchezaji wa timu ya mpira wa wavu ya
Jeshi Stars David Evarist kabla ya kuanza kwa fainali ya mashindano ya wazi ya
taifa ya wavu wa ufukweni dhidi ya Karafuu ya Zanzibar jijini Dar es Salaam.
Karafuu walishinda seti 2-0.
|
|
Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu
ya Karafuu ya Zanzibar Mohamed Ismail (kushoto) akiruka kupiga mpira, huku
mchezaji wa Jeshi Stars Ford Edward akijaribu kuuzuia wakati wa mchezo wa
fainali ya mashindani ya taifa ya wazi ya ufukweni uliofanyika juzi kwenye
hoteli ya Mbalamwezi Mikochini jijini Dar es Salaam. Karafuu walishinda 2-0.
|
Ahsante sana Image Power Media. Nawa pongeza kwa kazi nzuri mliyo fanya kwa kutangaza Black Energy National Beach Volleyball Tournament. Black Energy Team www.blacktz.com
ReplyDelete