Mtoto anayeugua ugonjwa wa Sikoseli, Nasma Khalid (wa
pili kushoto), akikikata keki wakati wa utambulisho wa Maadhimisho ya Siku ya
Sikoseli Duniani kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es
Salaam leo. Wanaongalia kutoka kushoto mstari wa nyuma ni; Mkuu wa Idara ya
Magonjwa ya Damu ya MNH, Dk. Stella
Rwezaura, Mratibu wa Tiba na Tafiti, Dk. Furahini Chinenere, Mratibu wa Upimaji
Sikoseli kwa Watoto, Dk. Deogratius Soka na baadhi ya watoto wanaougua
sikoseli. Siku ya Sikoseli Duniani huadhimishwa Juni 19 kila mwaka.
|