KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMA E-mail: dvdmwk6@gmail..com SIMU: 0713 084 360

Sunday, May 31, 2015

Sherehe za Uzinduzi wa Shule ya Sullivan Provost wafana

 Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Mlandizi, Mchungaji Tusimsahau Manoza (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan  Provost, Rachel Mwalukasa (wa tatu kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo mjini Kibaha Pwani juzi. Wengine kutoka kushoto ni Mwinjilisti Andrew Utoah wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Kidugalo, Mchungaji Liston Imaniyangulu Kiongozi wa Kiroho katika shule na Mkuu wa Shule ya Sullivan Provost, Jacob Isack Mkumbo.

 Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Mlandizi, Mchungaji Tusimsahau Manoza (kulia) akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost mjini Kibaha Pwani juzi. Wengine kutoka kushoto ni wajumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mhandisi  Dk. Ellen Kalinga na Prisca Michael Barnabas; Mkurugenzi wa shule hiyo, Rachel Mwalukasa na Mkuu wa Shule ya Sullivan Provost, Jacob Isack Mkumbo.

 Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Mlandizi, Mchungaji Tusimsahau Manoza (kulia) akilakiwa na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan  Provost, Rachel Mwalukasa alipokwenda kuzindua  rasmi jengo la shule hiyo mjini Kibaha Pwani juzi. Katikati ni Mwinjilisti Andrew Utoah wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Kidugalo mjini Kibaha.  Mchungaji

 Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa akikata keki kusherehekea miaka 50 ya kuzaliwa kwake tukio lililoambatana na shamrashamra za uzinduzi wa shule hiyo.

 Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa (kulia) akiwapa keki baadhi ya  watoto  wakati wa akisherehekea miaka 50 ya kuzaliwa kwake pamoja na tukio la uzinduzi wa shule hiyo.

 Baadhi ya wageni waalikwa wakimpongeza Mkugenzi wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa mara baada ya uzinduzi rasmi wa jengo La shule hiyo.

 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost wakiimba ili kunogesha sherehe hizo shuleni hapo.