BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA AKAUNTI ZA MISHAHARA.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa
ya Biashara (NBC), Andrew Lyimo (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Kampeni ya akaunti za mishahara iliyopewa jina la ‘Mcheza Kwao’ yenye lengo la kuhamasisha
wafanyakazi kuchukulia misharahara benki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter na Meneja
Malipo ya Mishahara na Maendeleo, Amos Lyimo.
Meneja Malipo ya
Mishahara na Maendeleo wa Benki ya NBC Tanzania, Amos Lyimo (kulia),
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya akaunti za mishahara iliyopewa
jina la ‘Mcheza Kwao’ yenye lengo la kuhamasisha wafanyakazi kuchukulia misharahara
benki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Kaimu
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NBC, Andrew Lyimo na Meneja Huduma za Jamii
wa benki hiyo, Irene Peter.
Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kushoto),
akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Idara ya
Wateja Binafsi, Andrew Lyimo na Meneja wa Malipo ya Mishahara na Maendeleo,
Amos Lyimo.
Baadhi ya waandishi waliohudhuria uzinduzi huo
wakisikiliza maelezo kuhusu kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo.