KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMA E-mail: dvdmwk6@gmail..com SIMU: 0713 084 360

Sunday, July 17, 2016

HUAWEI YAFUNGUA DUKA KUBWA MLIMANI CITY DAR ES SALAAM

Afisa ardhi (wilaya) Bagamoyo, William Ndesanjo kushoto akipokea simu mpya aina ya Huawei GR3 mara baada ya kununua katika Duka jipya Mlimani city lililofunguliwa rasmi na Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora hayupo pichani.

 

Baadhi ya wakazi wa jiji wakisubiri kushuhudia  uzinduzi wa Duka kubwa  jipya la Simu aina ya Huawei Mlimani city Dar es Salaam


 
kikundi cha Dancer wakifanya vituvyao wakati wa uzinduzi wa Duka jipya la Huawei Milimani city jijini Dar es Salaam.

 
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka jipya la simu za mkononi la Huawei, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akisalimiana na Naibu Balozi wa China nchini, Gou Haodong (kulia),  na katikati ni mkurugenzi mtendaji  wa Huawei nchini, Bruce Zhang, hafla hiyo ilifanyika mlimani city jijini Dar es Salaam.  

. Naibu Balozi wa China nchini, Gou Haodong (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kushoto)  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Duka jipya la Huawei jijini Dar es Salaam.

 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora katikati na Naibu Balozi wa China nchini, Gou Haodong (kulia) pamoja na mkurugenzi mtendaji  wa Huawei nchini, Bruce Zhang, kushoto, wakikata utepe kufungua rasmi duka jipya la Huawei lililopo mlimani city jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Huawei kulia akitoa maelezo ya simu mpya ya P 9lite kwa mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora wa tatu toka kulia pamoja nae ni Naibu Balozi wa China nchini, Gou Haodong na mkurugenzi mtendaji  wa Huawei nchini, Bruce Zhang mara baada ya kufungua duka jipya la Huawei Milimani city Dar es Salaam.
 
 
Mambo ya Huawei