Mkurugenzi
wa mafunzo kutoka baraza la habari Tanzania akizungumza na wanahabari
mapema leo kuhusu mchakato wa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari
nchini Tanzania
|
Baraza
la habari Tanzania leo wametangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa tuzo za
umahiri wa uandishi wa habari Tanzania mashindano ambayo yatakjuwa ni
mara ya sita kufanyika nchini Tanzania.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini dare s salaam mkurugenzi wa mafunzo kutoka
baraza la habari MCT Bi PILI MTAMBALIKE amesema kuwa katika mashindano
ya mwaka huu kuna mabadiliko kidogo ambapo amesema kuwa kuna makundi
ambayo yameongezwa katika nafasi zinazoshindaniwa ambayo ameyataja kuwa
ni gesi,mafutana uchimbaji madini na kundi la afya ya mama na
mototo.ambapo amesema kuwa makundi hayo yameongezwa kutokana na umuhimu
wake hapa nchini kwa sasa.
Tamasha
hilo ambalo limepangwa kufanyika mwaka mwakani mwezi wa tatu tarehe
24,2015 ambapo mtambalike amesema kuwa tuzo hizi zinalenga kuwatambua na
kuwatunza waandishi wa habari waliofanya kazi yao vizuri katika kazi
zao na makundi mbalimbali kushindaniwa
Mmoja kati ya waratibu wa shindano hilo Bi CHIKU LWENO akiielezea mikakati ya tuzo hizo kwa msimu huu
|
Makundi yatakayoshindanishwa mwaka huu ni uandishi wa habari za uchumi,habari,michezo na tamaduni,mazingira,afya, watoto,HIV/UKIMWI,utawala
bora,jinsia,sayansi na technologia,afya ya mama na
motto,uchunguzi,elimu,watu wenye ulemavu,utalii na uhifadhi,mpiga picha
gazeti,mpiga picha runinga,mchora katuni bora,uandishi wa habari za
kilimo,afya ya uzazi kwa vijana,pamoja na tuzo ya uandishi wa habari za
gesi,mafuta na uchimbaji madini,pamoja na kundi la wazi.
Bi
PILI MTAMBALIKE amewataka waanndishi wa habari kujitokeza kwa wingi
kupeleka kazi zao ili zishindanishwe na kupata mshindi wa tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment