Wadhamini wa shindano la Fanya Kweli Kiwanjani “Tusker Lager” mali ya Kampuni ya bia ya Serengeti wamemuibua mshindi wa tatu wa shindano hilo siku ya jumamosi baada ya mtanange mkali wa kuitafuta baa ya wiki uliofanywa na wadhamini hao wiki iliyopita.
“New
Jambo Bar” ya Mabibo, Ubungo ndiyo iliyobahatika kuzipiga kikumbo baa nyingine
9 zilizoingia kwenye mchakato huo wa kumpata mshindi wa wiki.
Kama
ilivyo ada siku ya jumamosi mameneja wa bia ya Tusker waliweka kambi katika
kiwanja cha New Jambo Bar ya Mabibo jijini Dar na kuporomosha burudani ya nguvu
sambamba na kugawa zawadi mbalimbali kama fulana, fedha taslim na bia za bure
kwa wapenzi wa bia ya Tusker hii ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa
wateja wa kinywaji hicho waliofika kupongeza ushindi wa baa hiyo.
Burudani
ya kuipongeza “New Jambo Bar” kama baa ya wiki ilianza mishale ya saa kumi na
moja na kudumu kwa takriban masaa sita. Burudani hiyo ya muziki ambayo ilikua
ikirushwa laivu na kituo cha redio cha E-fm ni muendelezo wa sherehe mbalimbali
zinazofanywa na Tusker kwenye baa mbalimbali za jiji la Dar ambazo zimeshinda shindano
la “Fanya Kweli Kiwanjani”.
Akiisifia
baa yake, alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari, Bw. Frank David Lema
ambaye ndiye Meneja wa baa hiyo alisema kuwa “Nimefurahi sana kwa watu wa
Tusker kututembelea kwenye baa yetu kwa kweli leo tumeuza kupita kiasi”. Kwa
kweli natamani hata wiki ijayo wangeendelea kuichagua tena baa yetu aliongeza
Meneja huyo huku akicheka na kumalizia kuwa wameuza chapa hiyo ya Tusker kuliko
siku zote tangu baa hiyo ifunguliwe
kutokana na wingi wa wapenzi wa kinywaji hicho.
Kwa
upande wake Afisa Mauzo wa SBL, eneo la
manzese – Mabibo, Bi. Anna Msomba ambaye alikuwepo kiwanjani hapo Bi. Sialouise
Shayo alisema kuwa “Tumefurahi kumpata mshindi wa tatu wa shindano letu, “New
Jambo baa” ni baa nzuri na ya kistaaarabu yenye wapenzi wengi wa Tusker na
nadhani hii ndiyo sababu kubwa ya watu kuipigia kura baa hii…Kampeni hii bado
inaendelea na tunatarajia zaidi ya baa 20 kuingia kwenye kinyang’anyiro hiki
kabla ya promosheni kufikia tamati”.
Bi. Msomba
aliendelea kuwasihi wadau na wapenzi wa bia ya Tusker kuendelea kuzipigia kura
baa mbalimbali zitakazo orodheshwa kwenye shindano hilo na kukumbushia kuwa ili
kuziwezesha baa za mitaa tunayoishi kuingia kwenye shindano hili wasisite
kusikiliza kipindi cha Ubaoni cha E-fm ambacho kinadadavua kwa undani kuhusiana
na promosheni hiyo.
Pamoja
na hayo, Meneja huyo alikabidhi Tsh. 100,000Tsh fedha taslim kwa wahudumu wa
baa hiyo kama zawadi kwa kufanya kweli kwenye upande wa kutoa huduma kwa siku
hiyo.