Droo ya mwisho ya kampeni ya Tutoke na Serengeti
imemshuhudia mkazi wa Korogwe Tanga Bw. Robert Gabriel Moriale akitangazwa
mshindi katika fainali ya kampeni “Tutoke na Serengeti”. Fainali hiyo
imefanyika katika ukumbi wa Baa ya Hongera iliyopo maeneo ya Kijitonyama-Dar es
salaam karibu na chuo cha Ustawi wa jamii.
Mshindi
huyo alijipatia fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo
ataongozana na mtu wake yeyote wa karibu kwa muda wa siku tatu huku SBL kupitia
bia yake ya Serengeti Premium ndio itahusika kugharamia usafiri, chakula,
malazi sambamba na fedha taslim za mshindi kujikimu pindi atakapokua safarini.
Akiongea kupitia njia ya simu mara baada ya kutangazwa
mshindi wa mtoko wa mbugani, Bw.Robert
(49)alipokea taarifa hizo kwa furaha na alisikika akishangilia kwa
kelele baada ya kuambiwa kwamba amejishindia “Mtoko wa Mbugani”.
Alipoulizwa kama alishawahi kushinda chochote
kabla ya zawadi hiyo, Robert alijibu “Nimekuwa nikishiriki tangu mwanzo na
nimepata bia za bure nyingi tu pamoja na pungozo la Tsh 300. Lakini hii ya leo
kwa kweli sikuitarajia kabisa”
Akiongea wakati wa kufunga kampeni hiyo, Meneja chapa
wa bia ya Serengeti Premium Lager , Bwana Rugambo Rodney alisema, “Tumefurahishwa
sana na ushindi wa bwana Robert na tunapenda kumshukuru kwa kushiriki na tunaamini
aliifurahia bia ya Serengeti Premium ambayo imemletea furaha ya kipekee siku ya
leo.
Rodney pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru
washiriki wote kwa kutumia muda wao wa thamani katika promosheni hii na kuwapa moyo wale ambao hawakubahatika
kushinda mtoko wa mbugani, Bajaj au bia za bure kutokata tamaa na kushiriki
tena nyakati zijazo kwani SBL imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kiasi
cha faida waliyopata kwa wateja wake. Aliongeza kuwa wateja wakae mkao wa kula
kwani kuna kitu kikubwa kinaandaliwa kwa ajili yao. Wakati kampeni hii iliyodumu takribani miezi minne
inafikia tamati, SBL imetoa shukrani za pekee kwa wateja wake wa Serengeti
Premium Lager baada ya kushuhudia washiriki
zaidi ya milioni moja wakijaribu bahati zao na kuifanya promosheni ya “Tutoke
na Serengeti” kuwa yenye mafanikio kutokana
na muitikio mkubwa na uelewa kutoka kwa wananchi.
Kampeni imewazawadia wateja mbalimbali fursa ya kutembelea
mbuga ya wanyama ya Serengeti wakati wengine wakiondoka na zawadi murua kama
vile Limo Bajaj ambazo kwa kiasi kikubwa zitabadilisha maisha yao. Kulikuwa pia
na fedha taslim za kila wiki, bia za bure, na punguzo la Tshs300 katika kila
bia ya Serengeti Premium.
Promosheni hii ya nchi nzima pia ilipata ushirikiano
wa hali ya juu kutoka kwa B-Pesa, wataalamu wa teknolojia mpya ya usambazaji
fedha waliochangia Limo Bajaj sita kwa washindi mbalimbali. Pia walihusika na
usambazaji wa fedha kwa washindi nchi nzima katika kipindi chote cha miezi mine
ya kampeni.
No comments:
Post a Comment