KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMA E-mail: dvdmwk6@gmail..com SIMU: 0713 084 360

Thursday, March 12, 2015

BENKI YA TAIFA YA BIASHARA (NBC) YAUNGANA NA SIKU NYA WANAWAKE DUNIANI KWA KUCHANGIA DAMU

 
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kushoto) akiwaongoza baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika tukio la  kujitolea damu lililoandaliwa na benki hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam.

 
Meneja Mahusiano ya Kibiashara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lukemelelo Kaduma (katikati) akijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa  NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami na kushoto ni mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Benard Elikana.

 
Mmoja wa wafanyakazi wa  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jolanda Songoro (kushoto) akijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa  NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami.

 
Meneja wa Idara ya Mikopo Midogo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jacob Samuel (kulia) akijitolea damu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa  NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami.

 
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, William Tendwa naye akishiriki tukio lililoandaliwa na benki hiyo la kujitolea damu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC wakijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi hao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam. Anayewatoa damu kushoto ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami.

 Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Bernard Elikana akiungana na baadhi ya wafanyakazi wa NBC kujitolea damu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kulia ni Petert Chami wa Damu Salama.

 
Mkazi wa Mwananyamala Dar es Salaam Subira Omar akijitolea damu katika tukio lililoandaliwa na Benki ya NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Anayemtoa ni Peter Chami kutoka Damu Salama (NBTS)

 
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, John Nyaindi  naye akishiriki tukio lililoandaliwa na benki hiyo la kujitolea damu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kushoto ni Daudi Mkawa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

 
Mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Peter Chami (kulia) akimuandaa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, Georgia Mwita ili aweze kumtoa damu katika  tukio hilo jijini Dar es Salaam.