KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMA E-mail: dvdmwk6@gmail..com SIMU: 0713 084 360

Sunday, March 29, 2015

BENKI YA NBC IDARA YA UENDESHAJI WAFANYA MKUTANO KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA BENKI

Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi zawadi kwa mfanyakazi aliyeitumikia benki hiyo kwa kipindi kirefu cha miaka 27, Said Kilala wakati wa  mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo (COO) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya

Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa jumla katika vipengele vyote wa  shindano la kumtafuta mfanyakazi mahiri  katika idara hiyo, Mwanaisha Ayosi wakati wa  mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya.

Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi wa shindano la kutafuta wafanyakazi mahiri katika idara hiyo, Emmanuel Simon wakati wa mkutano wa Idara ya Uendeshaji ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Everline Ugomba kutoka ofisi ya COO.

 
Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo (COO) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika mkutano huo wafanyakazi hao waliweza kuweka mikakati mbalimbali ya kufanikisha maendeleo ya benki hiyo.


 
Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (wa nne kushoto waliosimama) akipozi kwa picha na washindi na washiriki wa shindano la kutafuta watumishi mahiri katika vipengele vya Respect, Integrity, Service Excellence, Stewardship wakati wa mkutano wao jijini  Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment