Meneja Usalama
na Mazingingira wa Kampuni ya Saruji
Tanga, Leon Breedt (wa tatu kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 300
ya saruji kwa Diwani wa Kata ya Pongwe, Uzia Juma, iliyotolewa na kampuni hiyo
kusaidia ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kisimatui kilichopo katika kata hiyo.
Mifuko hiyo ina thamani ya shs milinioni 3.5. Hafla ya makabidhiano ilifanyika
kiwandani hapo, Pongwe, Tanga juzi. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Kiwanda,
Mhandisi. Ben Lema, Meneja Biashara, Matthews Roos, Ofisa Mtendaji Kata ya
pongwe, Salimu Mdoe, na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Samuel Shoo. |