KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMA E-mail: dvdmwk6@gmail..com SIMU: 0713 084 360

Monday, June 8, 2015

Benki ya NBC yatoa msaada wa madawati kwa Shule ya Msingi Mlingotini mjini Bagamoyo

 Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Molel (kulia), akikabidhi sehemu ya  msaada wa madawati 30 kwa mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mlingotini, Wediel Besha, yaliyotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Bagamoyo, Pwani

 Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Molel (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlingoti wakati akikabidhi msaada wa madawati 30 yaliyotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Bagamoyo mkoani Pwani.

 Meneja Mafunzo wa Benki ya NBC, John Nyaindi (kulia ) akikabidhi baadhi ya madawati kwa mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Mjaka Chamwamba wakati wa hafla hiyo.

 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlingoti wakifurahia baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati kutoka NBC na Mkuu wa Rasilimali Watu wa benki hiyo, Flora Molel (kulia).

 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlingoti wakipozi kwa picha na  Mkuu wa Rasilimali Watu wa NBC Flora Molel (nyuma kulia) katika hafla hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya shule, Mjaka Chamwamba (kushoto), na Mwalimu Mkuu wa shule ya Mlingotini, Wediel Besha.