Man City yathibitisha kumnasa Negredo |
Man City yathibitisha kumnasa Negredo
LONDON, England
WASHINDI wa pili wa Ligi Kuu ya England wamekamilisha usajili wao wa tatu katika msimu huu wa majira ya joto baada ya kumsajili mshambuliaji wa Sevella na Hispania Alvaro Negredo.
Huo ni usajili watatu kufanywa na vigogo hao wa soka Uingereza, ambapop tayari wameshamnasa mchezaji mwingine wa kiamtaifa wa Hispania Jesus Navas kutoka Sevilla aliyetua Etihad hivi karibuni.
Mtandao wa Goal Com ulibainisha kuwa, Man City imetoa kitita cha pauni Milioni 2.1, huku uongozi wa klabu hiyo ukithibitisha kusajiliwa kwa Negredo.
Mchezaji huyo alifunga mabao 63 katika mechi zake 95 alizoichezea Sevilla lakini sasa atavaa jezi namba 9 chini ya kocha mpya wa timu hiyo Manuel Pellegrini.
Huo ni usajili wa tatu chini ya kocha huyo mpya katika klabu hiyo yenye maskani yake kwenye uwanja wa Etihad.
Negredo anafuata nyayo za Fernandinho na mchezaji mwenzake wa Sevilla Jesus Navas, aliyejiunga na Man City akitokea Sevilla mapema mwezi huu.
"City wanafuraha kutangaza kumsajili Alvaro Negredo, ambaye anakuwa mchezaji watatu kusajili na klabu hii katika kipindi hiki cha majira ya joto, " ilisomeka taarifa ya klabu hiyo.
"Ataungana na wenzake katika kikoso ambacho sasa kipo katika ziara ya maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi, na atavaa jezi namba tisa."
Stevan Jovetic pia msimu uliopita alitaka kujiunga na washindi hao wa pili wa Ligi Kuu ya England baada ya klabu hiyo kukubali kulipa kiasi cha pauni Milioni 23.3 na klabu ya Ligi Kuu ya Italia ya Serie A ya Fiorentina, huku Pellegrini akiwa na njaa ya kukiongezea nguvu hasa katika safu ya ushabuliaji.
*********
Pellegrini aiacha Manchester City
KOCHA Mkuu wa Manchester United ameondoka na kurejea nchi kwao Chile na kuiacha timu hiyo Durban Afrika Kusini ambako ilikuwa ikifanya ziara ya majaribio kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England kwa sababu ya kifamilia.
Kuondoka kwa kocha huyo aliyejiunga hivi karibuni kumemfanya msaidizi wake Brian Kidd kuchukua kwa muda mikoba ya bosi wake ya kuinoa timu hiyo katika ziara hiyo ya Afrika Kusini.
Manchester City ilikubali kipigo kutoka kwa wenyeji wao Ama Zulu.
‘Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ameondoka kwa muda katika ziaya ya maandalizi ya timu hiyo na kurejea kwao Chilekutokana na matatizo ya kifamilia, “ilisema taarifa ya klabu hiyo.
Washindi hao wa pili wa Ligi Kuu ya England walithibitisha hayo katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo kuwa, kocha huyo hatakuwepo wakati wa mchezo wa Alhamisi dhidi ya AmaZulu nchini Afrika Kusini kutokana na kuondoka ghafla asubuhi hiyo.
Pellegrini anatarajia kuungana na kikosi hicho huko Hong Kong katika mchezo ujao wa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England.
***
Ratiba ya Ligi ya Mabingwa yapangwa
SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (UEFA), leo Ijumaa limepanga ratiba ya awali ya kufuzu kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Nafasi 30 zitagombewa katika hatua ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Mechi za ufunguzi zitachezwa Julai 30 na 31, ambapo zile za marudiano zitapigwa Agosti 6 na 7:
RAUNDI YA TATU YA KUFUZU KWA LIGI YA MABINGWA WA ULAYA:
Nordsjaelland (NOR) VS Zenit St Petersburg (RUS)
Salzburg (AUT) VS Fenerbahce (TUR)
PAOK (GRE) VS Metalist Kharkiv (UKR)
PSV (NED) VS SV Zulte Waregem (BEL)
Olympique Lyonnais (FRA) VS Grasshopper Club (SUI)
Basel (SUI) VS Gyori (HUN)/Maccabi Tel-Aviv (ISR)
Sligo Rovers (IRL)/Molde (NOR) VS New Saints (WAL)/Legia Warszawa (POL)
Slovan Bratislava (SVK)/Ludogorets (BUL) VS Shirak (ARM)/Partizan (SRB)
Dinamo Tbilisi (GEO)/Streymur (FRO) VS Steaua Bucharest (ROU)/Vardar (MKD)
APOEL (CYP) VS Birkirkara (MLT)/Maribor (SVN)
Celtic (SCO)/Cliftonville (NIR) VS Elfsborg (SWE)/Daugava Daugavpils (LVA)
BATE (BLR)/Shakhter Karagandy (KAZ) VS Neftci PFK (AZE)/Skenderbeu (ALB)
Austria Vienna (AUT) VS Ekranas (LTU)/Hafnarfjordur (ISL)
HJK Helsinki (FIN)/Nomme Kalju (EST) VS Viktoria Plzen (CZE)/Zeljeznicar (BIH)
Fola Esch (LUX)/Dinamo Zagreb (CRO) VS Sheriff (MDA)/Sutjeska (MNE)