KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMA E-mail: dvdmwk6@gmail..com SIMU: 0713 084 360

Saturday, April 11, 2015

NBC BENKI YAZINDUZUA HUDUMA YA BENKI NILIPO JIJINI DAR ES SALAAM.

 Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Maria Alina Kimaryo (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa (kushoto) na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canicius Joseph wakizindua huduma mpya  ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam. Wateja wa benki hiyo sasa wanaweza kupata huduma za kibenki kwa kutumia program maalum ya NBC katika ‘play store’ hivyo kupata huduma za kibenki kupitia laptop zao, tablets na simu za mkononi za smartphones.   

 Mshauri wa Bidhaa wa Benki ya NBC, Canisius Joseph (kulia), akionyesha jinsi huduma mpya ya NBC Benki Nilipo inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo, Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.  

 Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya NBC, Wambura John (katikati) akimwonyesha mmoja wa mteja, Nusra John (kulia) jinsi anavyoweza kutoa pesa katika ATM ya benki hiyo bila ya kuwa na kadi kwa kutumia huduma ya NBC Cash Popote katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.  



Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa  (kushoto), akizungumza wakati  wa uzinduzi wa huduma mpya ya  NBC Benki jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canisius Joseph.


 Meneja Mahusino wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akiweka mambo sawa katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.

 Mshauri wa Bidhaa wa Benki ya NBC, Canisius Joseph (kulia), akimwonyesha mmoja wa wateja, Amini Juma (kushoto), jinsi huduma mpya ya NBC Benki Nilipo inavyofanya kazi kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni  Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.  

 Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC wakishuhudia uzinduzi wa NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam.


 : Baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini ar es Salaam